Wednesday, 15 March 2017

Rais Magufuli ametengua uteuzi wa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu

Jana March 15, 2017 Rais Magufuli ametengua uteuzi na kumsimamisha kazi Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge) Uledi Abbas Mussa. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa kutenguliwa kwa uteuzi na kusimamishwa kazi kwa Uledi Abbas Mussa kumeanzia jana tarehe 15 Machi, 2017.
Hatua hiyo imechukuliwa ili kupisha uchunguzi zaidi dhidi ya Uledi Abbas Mussa kufuatia kutozingatiwa kwa taratibu zinazotakiwa katika kushughulikia masuala ya uwekezaji

MAGAZETI YA LEO ALHAMISI TAREHE 16/03/2017