Sunday, 10 April 2016

Alshabab wavamia kituo cha polisi Wajir Kenya



Wapiganaji takriban 100 wa kundi la kigaidi la Alshabab wamevamia kituo kimoja cha polisi Wajir Kaskazini mwa Kenya.
Hadi kufikia sasa idadi ya waliojeruhiwa ama kufa haijajulikana lakini kinachothibitishwa na serikali kuwa walifaulu kuteka gari la serikali aina ya Land Cruiser.
''wavamizi walishambulia kituo cha polisi cha Diff na wakakabiliwa vikali na askari waliokuwepo, wengi wao walijeruhiwa ila walifaulu kuteka nyara gari la serikali la kituo cha Diff ambalo walitumia kuwabeba majeruhi wao'' alisema Inspekta Jenerali wa polisi wa Kenya Joseph Boinnet.
Maafisa 3 wa polisi wa Kenya walijeruhiwa.
Kundi hilo lilitorokea mpakani.
Kikosi cha jeshi la Kenya limewafuata huko baada yao kuvuka mpaka kati ya Kenya na Somalia.

No comments:

Post a Comment