Thursday, 14 April 2016

WEMA SEPETU AMWAGA IDRIS SULTANI KISA MILIONI 98,MENGI MAZITO YAFICHUKA

wemaa-1Wema akiwa na Idris.
Waandishi wetu,Habari ya mtoto mzuri Wema Sepetu ‘Madam’ kumwagana na mpenzi wake, Idris Sultan si ngeni masikioni mwa wapenda ubuyu, imetapakaa kwenye mitandao ya kijamii lakini Amani limenasa sababu kubwa inayodaiwa kusababisha penzi hilo kuvunjika, twende pamoja.
Mwishoni mwa wiki iliyopita, wawili hao waliripotiwa kumwagana rasmi ambapo haikubainika mara moja sababu.
TUJIUNGE NA CHANZO
Iliposambaa habari hiyo, mapaparazi wetu waliingia kazini kuchimba zaidi ubuyu huo ambapo walifanikiwa kuzungumza na mmoja wa marafiki wa Wema ambaye alieleza siri ya wawili hao kumwagana.
“Kilichomfanya Wema amwagane na Idris si kingine ni shilingi milioni 98. Unajua Madam anadaiwa fedha hizo ili alikomboe lile gari lake (Range Rover Evoque) linaloshikiliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Sasa akamuomba Idris amlipie, jamaa akazingua. Hapo ndipo penye sababu kubwa iliyomfanya Wema amaindi hadi wakamwagana na Idris,” alisema shosti huyo wa Wema.
idriss sultanaIdris Sultan.
IDRIS ADAIWA KUFULIA
Akaendelea: “Nasikia Idris kwa sasa amefulia. Zile shilingi milioni 500 alizoshinda kwenye Shindano la Big Brother (Hotshot 2014) zote zimeyeyuka. Ameshindwa kumhudumia Madam, Wema ameona isiwe tabu, bora amuweke pembeni aangalie ustaarabu mwingine.”
GARI LILIVYOKAMATWA
Mapema mwaka huu, Wema akiwa katika mizunguko yake maeneo ya Mbezi Beach jijini Dar, alikamatwa na maafisa wa TRA waliokuwa wakifanya ukaguzi wa magari ambapo mrembo huyo alipotakiwa kuonesha vibali vya gari hilo ambalo awali alidai amejizawadia kwenye bethidei yake, hakuwa navyo na hata alipopewa muda wa wiki moja kuviwasilisha, hakuweza kufanya hivyo.
Baadaye, gari hilo lilishikiliwa na TRA ambapo walipoona Madam ameingia mitini, walianza kulinadi kwa shilingi milioni 98 hivyo mrembo huyo aliposikia, alimuomba Idris amlipie lakini jamaa inadaiwa alidunda.
SABABU NYINGINE
Chanzo kingine kilicho karibu na wawili hao kililieleza Amani kuwa mbali na shilingi milioni 98, sababu nyingine ambazo ni chanzo cha wawili hao kumwagana ni:
YA PILI
“Wema alikuwa hataki kufuatiliwafuatiliwa katika uhusiano wao. Kuna wakati Idris alizidisha kumfuatilia. Ilikuwa akimkosa kwake na kwenye simu, anamfuata kwa marafiki zake. Hata akijibiwa hayupo bado alikuwa anakwenda kwa rafiki husika kumtafuta.
“Kama mnakumbuka kuna kipindi alikuwa anakwenda kumfuata Wema hadi nyumbani kwa Aunt (Ezekiel). Sasa Madam ile kitu alikuwa hapendi.”WEMA2Mtoto mzuri Wema Sepetu ‘Madam’.
YA TATU
“Idris aligeuka kuwa tegemezi kwa muda mrefu. Wema mwanzoni hakushtukia, alitoa akiamini mapenzi ndivyo yalivyo lakini suala hilo lilipozidi nalo liligeuka kuwa kero. Wema anapenda akiwa na mtu kwenye uhusiano awe anamwagiwa mapesa kama vile ilivyokuwa kwa yule kigogo wake CK au Diamond.
YA NNE
“Sababu nyingine ni Idris kumzuia Wema kufanya matanuzi. Wema anataka akiwa nazo atumie sasa jamaa alipojifanya anajua kumpangia matumizi nalo lilikuwa tatizo. Madam unaanzaje kumbana kimatumizi kwa mfano?”
YA TANO
“Idris naye alimuona Wema kuhusu tukio lake la kupigana mabusu na yule mwanaume asiyeeleweka. Sasa kitendo hicho hakikumfurahisha Idris, akamchana ‘live’ Madam.”…
WEMA ANASEMAJE?
Alipotafutwa kuhusu sababu za yeye kummwaga Idris, Wema hakutaka kuingia moja kwa moja badala yake alifunguka kwa kifupi kuhusu sababu ya kupiga picha akiwa anambusu mwanaume huyo hivi karibuni.
“Ha! Ha! Haa! Davto tunazinguana tu na ni  mshikaji wangu kitambo… watu walikuwa kwenye pati and (na) tulikuwa tuna have fun (tunafurahia).”
IDRIS HUYU HAPA!
Jumatatu iliyopita, Amani lilimpigia simu Idris lakini hakupokea, alipotumiwa ujumbe mfupi wa maandishi kupitia Mtandao wa Instagram (Insta direct) kumuuliza juu ya yeye kumwagana na Wema pamoja na kufulia hadi kushindwa kumlipia Madam shilingi milioni 98, alicharuka na kuamua kujibu hadharani katika ukurasa wake wa Instagram.
“Nashangaa mwandishi kuniuliza kuwa nimefulia wakati sasa hivi mimi nipo vizuri kweli kweli. Nilifulia zamani na si sasa.”
“…mliokuja na skendo za Idris kuishiwa mbona mmechelewa sana? Mnazileta stori sasa hivi  wakati hela zimerudi… miezi minne nyuma zilipoisha mlikuwa wapi?”
Hata hivyo, taarifa za kufulia kwa Idris, zilitua kwenye dawati la gazeti hili siku nyingi nyuma lakini mwenyewe amekuwa akiwakwepa waandishi wetu, hivyo kufanya habari hiyo isiandikike kwa sababu za kitaaluma na kiweledi kwa kuwa haikuwa na mzani (balansi).
TUMEFIKAJE HAPA?
Idris alikipokea kijiti cha penzi la Wema mara baada ya kurejea Bongo akitokea Afrika Kusini akiwa amejishindia kitita cha shilingi milioni 500 kupitia Shindano la Big Brother.
Kabla ya hapo, mrembo huyo alikuwa akimilikiwa na staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ ambaye walimwagana na mshikaji huyo kuanza kutoka na Zarina Hassan ‘Zari’, mrembo kutoka Uganda.

No comments:

Post a Comment