Friday, 22 April 2016

Nay Wa Mitego kumsaidia mzazi mwenzie ‘Siwema’ Baada ya Kufungwa Jela.

Mahakama ya wilaya ya Nyamagana,Mkoani Mwanza jana ilimhukumu miaka miwili jela mzazi mwenzie na msanii Nay Wa Mitego, Siwema Edson kwa makosa ya kimtandao,msanii huyo anafikiria kuahirihisha shoo yake kwa mwisho wa mwezi huu ili aende Mwanza kumsaidia mama watoto wake huyo.
Nay wa Mitego akiwa na Siwema pamoja na mtoto wao zamani
Nay wa Mitego akiwa na Siwema pamoja na mtoto wao zamani
’Inabidi niondoke hivi karibuni ilibidi nisubiri nimalize shoo lakini kwa ajili ya kumpambania kwa ajili ya kwenda kujua ‘situation’ ya kule ikoje na pia wapi pa kuanzia,mwisho wa mwezi huu nina shoo mjini Sumbawanga lakini inabidi niende kwanza Mwanza nikafight suala la huyu bibie halafu nijue inakuwaje kama nita’cancel’ shoo au itakuwaje lakini hadi sasa hivi nawasiliana na ndugu zake kila mtu amekuwa kama amepagawa hivi hakuna anayejua wapi kwa kuanzia unajua kimekuwa ni kitu ambacho hakuna mtu aliyekuwa anategemea’’Alisema Nay Wa Mitego.
cloudsfm.com

No comments:

Post a Comment