Saturday, 16 April 2016

DIAMONDI ASHIKWA UCHAWI, AKUTWA NA FUVU LA BINADAMU






 Wakati mwenyewe akikanusha vikali kwamba hatumii ndumba kwenye muziki wake ambao sasa umemfikisha mbali kimataifa, staa wa Afro-Pop, Nasibu Abdul Jumaa ‘Diamond Platnumz’, ameshikwa uchawi kufuatia kukutwa laivu kwa fuvu linalodaiwa ni la binadamu ndani ya ofisi zake.
TUJIUNGE OFISINI KWA DIAMOND
Mapema wiki hii, vyanzo mbalimbali ambavyo ni wageni waliofika kwenye ofisi za mkurugenzi huyo wa Kampuni ya Wasafi Classic Baby (WCB), Diamond au Mond zilizopo Mapambano-Sinza jijini Dar, vilitonya kuwa, wengi walishtushwa na fuvu hilo baada ya kuliona mezani kwa mwanamuziki huyo.

MTOA UBUYU
“Haloo…Hapo ni Gazeti la Risasi tuwape ubuyu? Kuna ishu tumeishuhudia kwa macho yetu hapa ofisini kwa Diamond. Hata sisi imetushtua,” kilisema chanzo hivyo Risasi Jumamosi likataka kujua ni kitu gani?
Risasi Jumamosi: Ndiyo, hapa ni Risasi Jumamosi. Unamaanisha ofisi za Wasafi hapo Mapambano? Kuna ishu gani?

FUVU LA BINADAMU?
Chanzo: Ndiyo hapa WCB, kwanza Diamond mwenyewe yupo. Ukifika ofisini kwake, tena kwenye meza yake (Diamond) mwenyewe kuna fuvu la binadamu kabisa.
Risasi Jumamosi: Una uhakika ni fuvu la binadamu kweli au ni kitu kingine?
Chanzo: Jamani ni fuvu la binadamu kabisa lenye mifupa. Inawezekana ndiyo chanzo cha utajiri wake na skendo inayomkabili ya uchawi katika kazi zake. Ninyi fuatilieni mtapata ukweli.
RISASI JUMAMOSI KAZINI
Risasi Jumamosi: Oke tuachie tulifanyie kazi.

Baada ya kunyetishiwa ishu hiyo, gazeti hili lilituma shushushu wake ndani ya ofisi hizo ambaye alilishuhudia fuvu hilo likiwa mkono wa kushoto mezani kwa Diamond huku jirani yake kukiwa na picha ya mwanaye, Latiffah Nasibu ‘Princess Tiffah’ iliyokuwa kwenye fremu.

“Ni kweli kuna fuvu la binadamu mezani kwa Mond (Diamond) but (lakini) sikufanikiwa kulishika kwa mikono yangu,” alisema shushushu wetu.

SHUHUDA MWINGINE
Mbali na shushushu wetu, shuhuda mwingine aliyehudhuria hafla ya kusaini mkataba wa dili jipya alilosaini Diamond la Ubalozi wa Tomato Sauce ofisini kwake hapo alilithibitishia gazeti hili kuwepo kwa fuvu hilo lilozua gumzo kwa mashuhuda wachache wa tukio hilo.

“Hata mimi nimelishuhudia hilo fuvu kwa macho yangu wala sijasimuliwa na nina picha zake kwenye simu yangu (huku akiperuzi kwenye smartphone). Kiuweli limezua sana minong’ono. Baadhi ya watu wanadai ni mambo ya uchawi na wengine wanasema ni moja ya alama ya Freemasons (jamii ya siri inayohusishwa na utajiri). Unajua fuvu la binadamu ni moja ya Alama za Freemasons na kama unavyojua Diamond amekuwa akitajwatajwa.

“Wapo wengine wanadai labda mambo hayo ndiyo chanzo cha utajiri wa jamaa (Diamond) wa ghafla lakini yeye mwenyewe ndiye mwenye kuufahamu ukweli.
“Lakini unajua kunapokuwa na ishara kama hizi (kukutwa kwa fuvu) ni rahisi sana kwa mashabiki wake ambao ni wengi kuhusisha na huu utajiri wake unaotajwa kufikia (shilingi) bilioni nane kwa sasa,” alidai shuhuda huyo.

DIAMOND AFUNGUKA
Baada ya kupokea ushuhuda na madai hayo mazito ya Diamond kuhusishwa na uchawi na Freemasons kufuatia kukutwa kwa fuvu hilo ofisini kwake, gazeti hili lilimfuata Diamond ofisini kwake lakini alikuwa ametoka.

Alipotafutwa kwa njia ya simu alifunguka kwa kifupi huku akidai kuwa fuvu hilo ni pambo tu kama mapambo mengine.
“Ni urembo au pambo kama mapambo mengine, hakuna kitu kama hicho,” alisema Diamond na alipobanwa kueleza alikolitoa na gharama zake alisema:
“Usidanganyike, hakuna anayeweza kumuweka mtu juu zaidi ya Mwenyezi Mungu.

“Mimi naswali sana na namtegemea Mungu kwa kila kitu na kweli ananipigania.
“Unajua watu wengi wamekuwa wakizungumza oooh…natumia uchawi lakini ukweli ni kwamba maombi, ubunifu, juhudi na heshima ndivyo vitu vinavyoweza kumfanya mtu yeyote kupata mafanikio katika kitu akifanyacho au jambo alifanyalo.”

HUKO NYUMA
Mara kadhaa Diamond amekuwa akihusishwa na matumizi ya nguvu za giza katika kufanikiwa lakini amekuwa akisisitiza kuwa siri ya mafanikio yake ni kujituma, kutafuta fursa na kuipenda kazi yake ya muziki ili sanaa ya Bongo ifike mbali.


CHANZO: RISASI JUMAMOSI -GPL

No comments:

Post a Comment