KUFUTAIA kuwepo kwa taarifa kuwa Mwigizaji Aunt Ezekiel amempiga chini mpenzi wake Moses Iyobo, mrembo huyo ameibuka na kusema taarifa hizo hazina ukweli.
Akizungumza na paparazi wetu, Aunt alisema madai hayo ya kuachana na mpenzi wake huyo yanatengenezwa na watu wake wa karibu hivyo akijiridhisha, atawatumbua.
“Wanaowaza kuwa mimi na Mose tunatarajia kugombana leo au kesho wako kwenye ndoto kali sana kwa kuwa hatujawahi kuwaza wala kufikiria kuhusu kuachana kabisa, nimeshatonywa wanaoeneza umbeya huo soon nitawatumbua,” alisema Aunt.
Chanzo: GPL
No comments:
Post a Comment