Monday, 11 April 2016

GIGGY MONEY ASHINDANA NA WEMA SEPETU KWA SHAPE

Giggy MoneyGift Stanford ‘Gigy Money’.
MSANII anayechipukia kwenye ulimwengu wa filamu Bongo, Gift Stanford ‘Gigy Money’ ‘amejivua’ akili kwa kumtambia staa wa filamu Bongo, Wema Sepetu kuwa si chochote kwake kwani hawezi kumfikia kwa umbo lake hususan kalio.

wema sepetuu78Wema Sepetu.
Akipiga stori na kona ya Bongo Movies, Gigy ambaye pia ni ‘muuza nyago’ kwenye video za Kibongo alisema kuwa ana kila sababu inayomfanya kujitambia kwa umbo lake ambalo linawateka hasa wanaume wakware.
“Kuna siku kwenye kipindi kimoja cha runinga tulishindanishwa kati yangu na Wema nani mwenye kalio kubwa nikamfunika, hicho ni kigezo cha kwanza kuwa nina uwezo wa kumpoteza na sehemu nyingine,” alisema Gigy.

No comments:

Post a Comment