Maelezo ya mwanzo ya Tunda Man amesema
‘Tulikua tunatoka Njombe baada ya kumaliza show yetu na tukasema bora tusilale tuwahi kufika Dar,tumetoka Njombe saa 10 alfajiri mimi nikawa nasikia usingizi nikamwambia mwanangu hebu tuendeshe kidogo,kufika kijiji cha Idetelo kilomita kama 20 au 30 kabla ya kufika Mafinga tukiwa tumelala tukashtuka Gari inaingia porini tukasikia mshindo mkubwa gari imepiga puuuh Dereva hapo hapo akawa amefariki‘
Tunda Man anamalizia kwa kusema
‘Tulikua watu watano kwenye gari aliyekaa mbele na Dereva amevunjika mkono na nyama zimechanika,kuna mtu aliyekua nyuma mapafu yamepasuka,Mimi nipo poa,kwa sasa hivi tuko Mafinga hapa Hospitali ya Wilaya tunaangalia taratibu za kuchukua mwili tuupeleke Kilosa kwa ndugu zake,marehemu aliyefariki anaitwa Mussa lakini watu wengi wanamjua kwa jina la Man katuzo.
No comments:
Post a Comment