Saturday, 9 April 2016
MLINZI WA MGOMBEA UBUNGE CCM AUWAWA KIKATIKILI
Aliyekuwa Mgombea Ubunge jimbo la Vunjo Innocent Melleck Shirima
ALIYEKUWA mgombea ubunge jimbo la Vunjo (CCM), Innocent Melleck Shirima, amelitaka Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro kuchukua hatua za haraka kuhusu uchunguzi wa mauaji ya mlinzi wa nyumba yake iliyopo Marangu ambaye aliuawa kwa kuchomwa visu na watu wasiojulika.
Mauaji hayo ya kikatili ambayo haijajulikana chanzo chake, yalitokea wiki hii nyumbani kwa Melleck ambaye ni kada wa CCM.
Melleck alipeperusha bendera ya CCM katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana, katika Vunjo mkoani Kilimanjaro.
Akizungumza na Mtandao huu, Melleck alisema, kwa sasa anaishi kwa hofu kubwa kutokana na mauaji hayo ya kinyama kwa kuwa hajui yalimlenga huyo mlinzi pekee ama alikuwa anatafutwa yeye.
Alisema wasiwasi unakuwa mkubwa kwa kuwa wauaji hayo hao baada ya kukamilisha unyama huo hawakuchukua kitu chochote nyumbani kwake.
Akisimlia mkasa huo, Melleck alisea siku ya tukio hilo, ilikuwa awasili nyumbani kwake akitokea Dar es Salaam, lakini bahati nzuria akawa amepata dharura na hivyo akaahirisha safari yake.
"Kutokea mauaji hayo kumenipa hofu kubwa pamoja na familia yangu yote kwa sasa inaishi kwa hofu," alisema
Alisema siku ya tukio alikuwa akipokea simu za watu wengi kutoka jimbo la Vunjo ambako aligombea ubunge, zikimuuliza anatarajia kufika Marangu muda gani
Melleck alisema baada ya kupokea simu hizo aliwajibu watu hao kuwa alikuwa njiani kuelekea huko, ingawa ukweli ni kwamba wakati huo bado alikuwa Dar es Salaam.
Taarifa kutoka eneo la tukio zinasema, jeshi la polisi linaendelea kuwasaka wauaji hao ili waweze kufikishwa katika vyombo vya sheria.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment