May 10 2016 Mkuu wa wilaya ya kinondoni, Ally Hapi amefanya ziara ya kushtukiza asubuhi na mapema majira ya saa kumi na mbili katika hospitali ya Sinza Palestina na kujionea changamoto zinazoikabili Hospitali hiyo.
Baadhi ya changamoto ambazo amezikuta Hospitalini hapo ni pamoja na wagonjwa kukosa neti kwenye vitanda, upungufu wa dawa na kukosekana kwa jenereta lenye nguvu la kuendeshea vifaa vinavyotumia umeme mwingi hivyo kushindwa kutoa huduma pindi umeme unapokatika.
Mkuu huyo wa wilaya anatarajia kukaa na uongozi wa Hospitali zote za serikali zilipo wilaya ya kinondoni kuona namna ya kutatua changamoto zinazowakabili.
CREDIT: MILLARD AYO
No comments:
Post a Comment