Mtu ama watu wasiojulikana wametega bomu la kienyeji katika canteen ya kituo cha polisi Nyakato.
Canteen hiyo ya polisi ipo karibu na kituo ambapo mfanyakazi wa eneo hilo Bi Sara jana majira ya saa mbili usiku wakati anakusanya chupa tupu aliona mfuko wa rambo chini ya meza akadhani mteja ameusahau hivyo akauchukua na kuutunza kaunta.
Meneja kabla ya kwenda kuutunza stoo mfuko huo majira ya tano usiku aliamua kuufungua kujua kuna nini na ndipo aligundua kuwa mzigo ule ulikuwa ni bomu lililotengenezwa kienyeji.
Bomu hilo lilitengenezwa kwa mchanganyo wa baruti, mbolea ,chupa mbili za konyagi zenye petroli na vipande vya chuma mithili ya goroli, ikiwa na betri mbili aina ya tiger na simu ndogo aina ya tecno kama kiwashio.
Bomu hilo la kienyeji halijaleta madhara kwani lilikuwa disconnected mapema.
No comments:
Post a Comment