Jerry Kato aliyedai kuzaa na mama Diamond.
STORI: Issa Mnally na Mussa Mateja, Ijumaa
Dar es Salaam: Kumekuwepo na usiri juu ya baba wa mdogo wa Mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Esma Platnumz lakini huenda utata ukafika mwisho baada ya aliyekuwa DJ maarufu jijini Dar kuibuka na kudai kuwa ndiye aliyemzaa mtoto huyo na mama Diamond, Sanura Kassim ‘Sandra’ akimpinga na kuamua kumuweka wazi baba halali wa Esma.
Esma Platnums
ILIKUWAJE?
Mapema wiki hii, mtu mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Jerry Kato mkazi wa Boko jijini Dar, alipiga simu kwenye chumba cha habari cha gazeti hili na kueleza kuwa, ana jambo linaloutesa moyo wake na kwamba amekuwa akitafuta kuwasiliana na Magazeti ya Global kwa muda mrefu hivyo angependa kukutana na mwandishi wetu ili atoe lililoukamata moyo wake.
WAKATUNA BOKO
Baada ya kufanyika mawasiliano, mwandishi wetu na Jerry walikutana na jamaa huyo huko Boko, nje kidogo ya Jiji la Dar ambapo alifunguka kuwa, yeye ndiye baba mzazi wa Esma Platnumz ila anashangaa mama wa mtoto huyo amekuwa akikwepa kumtambulisha.
Diamond na mama yake Sanura.
MSIKIE MWENYEWE!
“Mimi naitwa Jerry Kato, nakumbuka mwaka 1982, nilikutana na huyu Sanura (Mama Diamond) pale Mbowe Hotel (sasa Bilicanas iliyopo Posta jijini Dar). Alikuja na jamaa mmoja anaitwa Spencer wakati mimi nafanya kazi ya U-DJ pale, tukatokea kupendana na kuanzisha uhusiano.
“Baada ya muda mrefu, Sanura alinasa ujauzito wakati huo mimi nakaa palepale Mbowe Hoteli, yeye anakaa Saigon (Kariakoo, Dar). Basi akawa anakuja pale hotelini na kunisumbua, si unajua tena mambo ya mimba.
“Kuna siku akaja na kuniambia anataka nimpe nauli aende Kigoma kwenda kujifungua, mimi sikuwa na kitu, nikamfuata bosi wangu Mbowe (Freeman), akampa nauli na kuondoka. Wakati huo hakukuwa na simu za mkononi, nikampa namba ya simu ya mezani ya pale hotelini.
“Tangu alipoondoka hakunipigia simu. Nikawa nakwenda kwao pale Saigon kuulizia, nikaambiwa ameshajifungua lakini jinsi ya kumpata sina. Nikaamua kuendelea na maisha yangu.
“Ikapita kama miaka 17 bila mawasiliano wala kuonana, sasa siku moja miaka kama miwili iliyopita nilikutana na jamaa mmoja akaniambia Sanura ananitafuta ila kaambiwa nimekufa. Kweli siku hiyo nikapewa namba yake na nikaongea naye akiwa Kinondoni.
“Akaniambia alikuwa ananitafuta lakini aliambiwa nimekufa. Basi tukapanga tuonane, akaniambia niende mpaka Sinza (Mori) pale Big Bon, nikifika pale nimpigie simu atanifuata.
“Mimi nikamchukua rafiki yangu mmoja ambaye anaijua historia yetu, tukaenda mpaka pale na kweli akaja kutuchukua na kutupeleka kwake. Mpaka nafika pale mimi sikuwa nikijua kuwa ndiye mama wa Diamond.
“Mara akaanza mazungumzo na kuniambia, ‘Jerry unakumbuka?’ nikamwambia nakumbuka, basi akaniambia, ‘sasa leo nataka nikuoneshe mtoto wako’. Akaita Esmaaa…, yule binti akaitika, akaja, akaita tena Nasibuuu, ndiyo akatokea Diamond akiwa ameshika simu yake akiwa kifua wazi.
“Hapo ndiyo akafanya utambulisho kwa Esma na kumwambia mimi ndiye baba yake hivyo asimsumbue tena. Na kweli nilipomtazama (Esma) anafanana na mama yangu mzazi hata rangi. Ikawa ni furaha tukakumbatiana na maisha yakaendelea.
MAWASILIANO KAMA KAWA
“Baada ya hapo mawasiliano yakawa yanaendelea, mimi naendelea na kazi zangu. Sasa kuna siku nikapiga simu kujua hali yao, yule mama akaniambia nisimpigie tena simu.
“Ikawa sasa kila nikipiga simu sipokelewi, hata mwanangu naye akawa hanipokelei. Nikaumia sana lakini nikaona sawa, baba ni baba tu. Kilichoniuma sasa ni baada ya kuona yule mtoto anaitwa jina la baba mwingine.
“Ndiyo maana nikaona nije niweke wazi ili watu wajue. Ninachotaka siyo mali zao ila mwanangu. Natoa habari hii ili kama atabisha basi twende tukapime DNA. Ila kiukweli kabisa yule alitakiwa kuitwa Esma Jerry Kato. Kwa hiyo ni hilo,” alidai mbaba huyo anayeonekana enzi zake alikuwa tozi ile mbaya.
MAMA DIAMOND ANASEMAJE?
Baada ya mzee huyo kuongea mengi, Ijumaa lilifanya jitihada za kumtafuta Mama Diamond ambapo alipopatikana aliamua kuanika siri ambayo huenda wengine walikuwa hawaijui.
“Daah! Kwanza hizo habari zimenishangaza sana, huyo Jerry simjui labda kwa wale wasiojua ni kwamba, baba wa Esma anaitwa Abdulkadiri, zamani alikuwa akiishi Dubai lakini sasa yupo Zanzibar kwa hiyo kama aliyekuja hapo kwenye magazeti yenu anaitwa jina hilo basi hakuna shaka ila nasisitiza tena kwamba huyo Jerry Kato simjui kabisa,” alisema mama Diamond.
Ijumaa lilijaribu pia kumpigia simu Esma ili kumuuliza kama anamjua mzee huyo lakini simu yake iliita bila kupokelewa.
CHANZO: GPL
No comments:
Post a Comment