May 12 2016 taarifa za kifo cha msanii wa filamu za Comedy James Petro Nsemwaambaye wengi tunamfahamu kwa jina la ‘Kinyambe’ zilianza kusambaa katika mitandao ya kijamii, kwa baadhi ya watu maarufu na wasanii kupost picha na kuonesha kuguswa na taarifa za kifo chake.
Ripota wa millardayo.com alifanikiwa kufika Uyole Mbeya na kukutana na baba mzazi wa marehemu mzee Petro Lugendelo Nsemwa na kutueleza nini kimepelekea kifo chaKinyambe ” Marehemu alikuwa anaumwa kwa kipindi cha miezi nane, alikuwa anasumbuliwa na pafu la upande mmoja lilikuwa alipumui vizuri”
Kingine ambacho hufahamu ni kuwa ndani ya mwezi mmoja yaani siku kadhaa kabla yaKinyambe kufariki alimpoteza mtoto wake wa mwisho Bray James Petro aliyekuwa na umri wa miaka minne, ila jana May 11 2016 ndio alifariki baba mtu yaani Kinyambe. Jina halisi analotambulika katika familia yake ni James Petro Nsemwa na sio Mohammed Abdallah kama ambavyo wengi wanafahamu.
No comments:
Post a Comment