Tuesday, 17 May 2016
JACKLINE WOLPER AFUNGUKA JINSI ANAVYOMZIMIA HAMONIZE MPAKA KUFA
Ama kweli penzi ni kikohozi, kulificha huwezi. Baada ya usiri mzito kutawala, hatimaye imebainika kuwa The Big Boss wa Wasafi Classic Baby (WCB), Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ndiye ‘aliyeinjinia’ penzi jipya mjini la muigizaji Jacqueline Wolper na kijana anayekuja kwa kasi kwenye Bongo Fleva, Rajabu Abdulhan ‘Harmonize’.
RISASI LILIANZA KUTONYWA
Awali, gazeti hili lilitonywa kuhusu penzi hilo jipya na chanzo chake makini na kueleza namna ambavyo Diamond alivyokuwa na mchango mkubwa katika kufanikisha Hamonize ambaye ni memba wa WCB ‘anamng’oa’ Wolper. “Diamond ndiye aliyesimamia mchakato mzima. Katumia kila mbinu kuhakikisha Wolper anaingia kwenye himaya ya mdogo wake. Nafikiri pia atakuwa ameangalia na suala zima la kibiashara, muziki sasa hivi unataka msanii azungumzwe,” kilisema chanzo hicho.
DOGO NDIYE ALIANZA KUSUMBUA
“Hamonize ndiye aliyeanza kuvutiwa na Wolper. Akamwelezea Diamond hisia zake, kama unavyojua tena Diamond si mtu wa kuremba, fasta tu akaweka mambo sawa. Kila kitu kikaenda kwenye mstari,” kilisema chanzo chetu.
MKONGO HANA CHAKE
Chanzo hicho kilizidi kumwaga ubuyu kuwa, kutokana na Diamond kumwaga ‘sumu’ za kutosha na Wolper kuingia penzini ‘mzimamzima’ ndani ya muda mfupi, Mkongo aliyekuwa anammiliki mrembo huyo hana tena chake kwa sasa. “Aaah! Mkongo hana chake tena kwa sasa. Wolper hasikii wala haoni. Amechanganyikiwa na penzi la Hamonize kiasi ambacho hataki kusikia habari ya mwanaume mwingine yeyote,” kilisema chanzo hicho.
MAMBO HADHARANI MITANDAONI
Mara baada ya chanzo hicho kumwaga ubuyu huo, wakati Risasi Mchanganyiko likiendelea kufanya uchunguzi wake, ghafla likakumbana na video ya wawili hao kupitia mtandao wa kijamii wa ‘Snap Chat’ ambayo ilimuonesha Wolper akiwa ‘hajiwezi’ kwenye gari akiimbiwa wimbo wa Number One wa Diamond na Hamonize aliyekuwa akiendesha gari hiyo.
WOLPER AJILIPUA
Bila kupoteza muda, Risasi Mchanganyiko lilimvutia waya Wolper ambaye bila hiyana alieleza jinsi gani alivyofika ‘Kigoma, mwisho wa reli’ kwa Hamonize ambapo alimmwagia sifa bwa’mdogo huyo kwa kudai hajawahi kupenda kama alivyompenda staa huyo anayetamba na wimbo wa Bado.
“Tena mimi naona kuwa sio mpenzi nambatiza jina la mume kabisa, maana nampenda mpaka kufa kuna wakati sijielewi ni mapenzi ya aina gani haya jamani na ninajuta kwa nini sikuingia huku mapema mpaka nikaanza kuhangaika kwa matapeli wa mapenzi.
ACHOMOA KUHUSU DIAMOND KUHUSIKA
“Hahaha siyo Diamond bwana aliyetuunganisha. Unajua mimi nilikuwa napata ujumbe kutoka kwa
marafiki zangu wa karibu kuwa Harmo ananipenda lakini nikawa bado sijaamua kuingia kwenye mapenzi, na hata tulivyoanza rasmi alikamilisha furaha yake kwani alifanikiwa kufunguka mwenyewe, nikamuelewa,” alisema Wolper.
AMFUNGUKIA MKONGOAlipoulizwa kuhusu mpenzi wake Mkongo aliyekuwa akifahamika na wengi hususan baada ya kuzagaa kwa picha zinazomuonesha akivalishwa naye pete ya uchumba, Wolper alisema huko ameshapita, alidanganywa vya kutosha: “Nilikuwa nadanganywa sana, kumbe nilikuwa na mtu ambaye tayari ana mke wake hivyo sikuwa na budi zaidi ya kulivua pendo kwake.
AZIDI KUJILIPUA
Kama hiyo haitoshi, Wolper alizidi kufunguka kuwa hatosikia la mtu kuhusu Hamonize, watakuwa pamoja kwa maisha ya tabu na raha kwani ndiye mtu ameweza kumponya vidonda vya Mkongo kwa haraka sana hivyo hatohangaika tena. “Sasa hivi sitojali chochote kwa kweli kwa maana Hamonize ndiyo ameweza kuponya vidonda vyangu kwa haraka sana nitakuwa naye katika hali yoyote shida na raha tutasonga tu,” alisema Wolper.
HARMONIZE HUYU HAPA
Risasi lilimvutia waya Hamonize ili kuweza kumsikia naye anazungumza nini kuhusu kukabidhiwa moyo na Wolper, aling’aka na kumuachia swali mwanahabari kisha kukata simu. “Kwani mmeshawasiliana na Wolper?” Alipopigiwa tena, alijibu: “Mbona amesema hajaongea na nyinyi?”
DIAMOND JE? Jitihada za kumpata Diamond ili aweze kuzungumzia penzi hilo jipya na namna alivyohusika kuunganisha ‘mambo’ hazikuzaa matunda baada ya kupigiwa simu saa 7, 7:45, 8:15, 9 na saa 10 jioni juzi Jumatatu lakini muda wote ilionekana imezimwa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment