12
Siku kadhaa zilizopita Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akijibu suala la Mbunge wa Monduli kuhusu umiliki na uporaji wa ardhi unaofanywa na baadhi ya watu hasa waliopo serikali katika jimboni humo, Waziri Lukuvi alieleza kuwa ni kweli kuna mashamba yaliyotakiwa kurudishwa kwa wananchi lakini hadi sasa bado.
Aidha aliendelea kusema shamba la Makuyuni ambalo lilidhaminiwa na Rais Benjamin Mkapa ili wapewa wananchi katika jimbo la Monduli, lakini aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa alijimilikisha na Waziri Lukuvi aliahidi kulirejesha mikononi mwa wananchi.
Kwa upande mwingine wa tuhuma hizo, Edward Lowassa amejibu na kusema kuwa halijui shamba alilolizungumzia Waziri Lukuvi na hakuna ardhi ambayo anaimiliki kinyume cha taratibu.
Aidha alitanabaisha kuwa hana taarifa kamili za suala hilo ila amemuomba Mbunge wa Mondulu Julius Kalanga kilifuatilia ili aweze kumpa taarifa kamili juu ya suala hilo ndipo ataweza kulizungumzia kwa mapana.
“Nashindwa kutoa maelezo kuhusu taarifa zaidi kwa sababu sifahamu lolote kuhusu shamba hilo. Mimi sipo Bungeni, ila nimesikia hizo habari hizo. Lakini nimemuomba Mbunge wangu analifuatilie kwa sababu sina shamba nilalolimiliki kinyume cha taratibu,” alikaririwa Edward Lowassa akizungumza na gazeti la JAMBOLeo.