Vikosi vya ulinzi na usalama Dar es salaam vimekamata mifuko ya sukari katika ghorofa linalojengwa maeneo ya Kinondoni baada ya kuripotiwa kufichwa na mfanyabiashara mwenye asili ya asia.
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda pamoja na mkuu wa wilaya Kinondoni Ally Hapi walifika kwenye eneo ambapo kwenye video fupi hapa chini Paul Makonda anaonekana akimuhoji mmiliki wa jengo hili.
Mmiliki wa jengo hili amesema sukari hiyo sio ya biashara bali ni kwa ajili ya misaada na amekua akiwapa watu ambapo pamoja na majibu hayo Makonda ameagiza jeshi la Polisi kuendelea kumhoji.
Kwenye hizi video mbili hapa chini wanaonekana Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Ally Hapi mapema kwenye jengo zilikoonekana sukari hizo na video ya chini yake anaonekana Mkuu wa mkoa Paul Makonda akimuhoji Mfanyabiashara mwenye asili ya asia ambaye ndio mmiliki wa jengo hilo Kinondoni.
CREDIT: MILLARDAYO
No comments:
Post a Comment