YANGA
ni mwanafunzi ambaye baba anajitaidi kununua vitabu vya kila aina ili mtoto wake afanye vizuri shuleni ,pia mwanafunzi anajitaidi pia kusoma kwa bidiii na anafaulu mitiani yake na kushika namba moja darasani wanafunzi wenzake wanamchukia cn kwa sababu anasifiwa cn na waalimu wake kutokana na mafanikio yke.
SIMBA
baba hana uwezo kwa sasa ila zamani alikuwa nao basi mwanafunzi anajivunia historia ya familia yake kwa zamani wazaz wake na ndugu zake walikuwa wasomi na y eye anafikiria atapata mafanikio kupitia historia ya familia yake ,hii hali inamfanya kila cku mwanafunzi hyu kuendelea kufanya vibaya pia anawaonea wivu wenzake wanaofanya vizuri na kusema wananunua mitiani.
AZAM,
baba tajiri anatimiza mahitaji yote ya mwanafunzi na malengo yke ni mtoto wake afike mbali kimasomo pia baba anatafuta twisheni mpaka nje ya nchi ili mwanae afanye vizuri lkn wapi mwanafunzi anabweteka na utajiri wa baba yake yeye asome asisome poa tu ,kitendo hk kinamfanya mwanafunzi hyu kuboronga masomo yake shuleni.
MTIBWA.
baba ni tajiri ameuza kila kitu ili mtoto afanye vizuri lakini mwanafunzi hazinduki tuuu anafuraia nafasi anayoishika lkn baba hafurahii hta kidogo lkn mwanfunz akifaulu mtiani mmoja tuu darasani anajiona yeye ni mkali cn baba amekata tamaa na mtoto hyu na amemwacha afanye anavyofanya yeye atakujajutia mbeleni.
COST UNION,
ni mwanafunzi wa ajabu cn hana jitiada darasani lkn ana mitiani yake na huwa lzima afaulu lkn kiburi chake cha kuchagua masomo machache tu huku akipuuzia masomo mengine kimemponza na atarudia darasa msimu uja.
KAGERA SUGAR,
Huyu mwanafunzi baba yake ana uwezo wa kawaida,mwanafunzi anahamahama cna shule ili aweze faulu bilakujua kwamba jitiada zke binafsi ndizo zitakazomwezesha afanye vizuri shuleni pia ana hatari ya kurudia darasa kwani maksi zke si nzuri kwa sasa
Hizo ni baadhi tu ya timu za bongo kama umependa na wewe endeleza hapo zilizosalia.
No comments:
Post a Comment