Thursday, 5 May 2016

KESI YA LULU KUSIKILIZWA MWAKANI - 2017


Kesi ya staa wa sinema za Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ya kudaiwa kumuua bila kukusudia msanii mwenzake, Steven Kanumba huenda ikaanza kusikilizwa mwakani (2017), Amani limeambiwa.


 Kwa mujibu wa chanzo kilichopo Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam inayosikiliza keshi hiyo, japo wananchi wengi wamekuwa wakisubiri siku ya kesi hiyo kusomwa lakini ukweli ni kwamba hakuna dalili yoyote ya kuanza kusikilizwa mwaka huu kwa vile mahakama hiyo ina kesi za watuhumiwa walioko mahabusu hivyo kuwamaliza kwanza hao. “Kesi ya Lulu kwa mwaka huu msahau kabisa. Hii kesi kutajwa labda kuanzia mwakani maana hakuna dalili yoyote na haipo kwenye listi ya kesi za mwaka huu. 
 
“Wale ambao walikuwa na shauku ya kujua kitakachojiri, hayo mambo ni mwakani maana mpaka sasa kesi ambazo zinapewa kipaumbele ni za watuhumiwa ambao wapo mahabusu magerezani.  “Ujue kuna kesi nyingi ambazo hazijasikilizwa.

 Kwa hiyo hizo ndo’ zinapewa nafasi ya kwanza kuliko kesi kama ya Lulu ambaye yupo nje kwa dhamana,” kilisema chanzo hicho. Ili kujiridhisha, gazeti hili lilimtafuta wakili wa msanii huyo, Peter Kibatala ambaye alijibu kwa kifupi: “Binafsi sifahamu kuhusiana na hilo, mpaka sasa sijajua hiyo kesi itakuwa lini kwa sababu sijaona ikipangiwa siku.”

No comments:

Post a Comment