Wakati wadau wa muziki wakifahamu kuwa msanii wa muziki wa Hip Hop Bongo, Rashid Makwilo ‘Chidi Benz’ yuko katika kituo cha kusaidia waathirika wa madawa ya kulevya ‘sober house’ kilichopo Bagamoyo mkoani Pwani, inadaiwa Chidi Benz alishatoroka kitambo na sasa yuko kitaa.
Akizungumza na Global Publishers meneja wa kituo hicho, Tumaini Majura, amethibitisha kuondoka kwa Chidi akiwa bado anaendelea kupatiwa matibabu.
“Ni siku 28 tu alikaa, lakini alitakiwa kukaa kwa muda wa angalau miezi mitatu ili kurudi katika hali yake ya kawaida,” alisema Tumaini.
Aliomgeza, “Nafikiri ni uamuzi wake binafsi maana siku moja meneja wake (Babu Tale) alikuja kumjulia hali, alipotaka kuondoka aling’ang’ania kuondoka naye. Sisi pamoja na Tale tulimsihi sana kubaki lakini alikataa,”
Pia Global walimtafuta Chid Benz, alipopatikana alikataa kuzungumzia suala hilo huku akisisitiza kuwa lolote kuhusu yeye atafutwe Babu Tale.
Tabu Tale alipoulizwa kuhusu mwala hilo alisema: “Sitaki kusikiliza wala kuzungumza lokote kuhusu Chid, muda ukifika nitaongea ila kwa sasa niacheni tu.”
No comments:
Post a Comment