AY akiwa na mwanasheria wake Alberto Msando nje ya Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam
Mahakama Kuu ya Tanzania leo imesikiliza mapingamizi ya awali ya maombi
ya rufaa yaliyowasilishwa na kampuni ya mawasiliano nchini Tigo dhidi ya
hukumu iliyotolewa na mahakama ya wilaya ya Ilala, April 11 mwaka huu
ya kutakiwa kuwalipa AY na Mwana FA shilingi bilioni 2.18 kama fidia ya
kutumia nyimbo zao bila ridhaa yao.
Mapingamizi hayo matatu yamewasilisishwa na Mwana FA na AY kupitia
mwanasheria wao, Alberto Msando. Miaka minne nyuma, wasanii hao wawili
walifungua kesi ya madai dhidi ya kampuni ya Tigo baada ya kutumia
nyimbo zao ‘Dakika Moja’ na ‘Usije Mjini’ kama miito ya simu kwa wateja
wake bila kuwa na mikataba nao.
Ijumaa hii, Mhe. Isaya Arufani ambaye ni Naibu Msajili wa Mahakama ya
Tanzania alisikiliza utetezi kutoka kwa mawakili wa pande hizo mbili.
Mwana FA na AY walikuwepo pia mahakamani hapo.
Mhe. Arufani ametaija June 27 kuwa siku ya kusikilizwa kwa maamuzi ya Mahakama Kuu kuhusiana na rufaa hiyo.
Mhe. Arufani ametaija June 27 kuwa siku ya kusikilizwa kwa maamuzi ya Mahakama Kuu kuhusiana na rufaa hiyo.
Alberto Msando akizungumza na mwanasheria wa kampuni ya Law Associates inayoiwakilisha kampuni ya Tigo kwenye kesi hiyo
“Kilichokuwepo leo ni kusikilizwa kwa mapingamizi ya awali ya maombi
waliyoleta Tigo ya kuomba kwamba kuzuia kukaza hukumu iliyotolewa na
mahakama ya Ilala. Kwahiyo leo tumesikilizwa mapingamizi hayo na
mahakama itatoa maamuzi yake tarehe 27 mwezi wa sita kuhusu mapingamizi
ambayo tumeyaweka dhidi ya maombi yao,” Alberto Msando, mwanasheria
anayewawakilisha AY na Mwana FA ameiambia Bongo5 mahakamani hapo.
“Yalikuwa mapingamizi matatu kwamba maombi yao yamekiuka baadhi ya vifungu vya sheria,” aliongeza Msando.
AY na Mwana FA wakiwa na mwasheria wao, Alberto Msando
Kwa upande wake Rosan Mbwambo wa kampuni ya Law Associates
inayoiwakilisha Tigo kwenye kesi hiyo amedai kuwa kampuni hiyo
haikuridhika na hukumu iliyotolewa na mahakama ya wilaya ya Ilala ndiyo
maana imekata rufaa.
“Sheria inaruhusu ukishakata rufaa uombe hukumu isitekelezwe mpaka rufaa
isikilizwe. Tigo wanasema tu wao hawajaridhika na kwasababu mfumo wa
kimahakama unaruhusu mtu asiporidhika kwenda juu, wameenda juu tu kwa
kuomba mahakama ya juu iangalie upya,” alisema Mbwambo.
Katika hukumu ya awali iliyotolewa na Hakimu Mfawidhi wa mahakama ya
Ilala, Juma Hassan, Tigo walitakiwa kulipa shilingi milioni 25 zingine
kama fidia kutokana na hasara waliyoipata wasanii hao kwa kutumiwa kwa
nyimbo zao. Hiyo imekuwa hukumu kubwa zaidi kuwahi kutolewa kwenye kesi
zinazohusiana na haki miliki za kazi za muziki nchini Tanzania.
No comments:
Post a Comment