Hamida Hassan na Mayasa Mariwata, Ijumaa
LICHA ya kukana kuwa hakufika kwenye pati ya sherehe ya kuzaliwa ya mama yake Wema, Mariam Sepetu iliyofanyika katika ukumbi wa Samaki Samaki, Masaki jijini Dar es Salaam juzikati, inadaiwa kuwa Idris Sultan, mtangazaji wa Kituo cha Redio cha Choice FM, ambaye ni mpenzi wa sasa wa muigizaji nyota Wema Sepetu, alizuiwa getini kuingia ndani ya ukumbi, kisa na mkasa, Ijumaa lina kila kitu.
Kisikie chanzo
Chanzo chetu cha kuaminika ambacho kipo karibu na mastaa hao kilitutonya kuwa, siku ya tukio hilo ambalo mastaa kibao walialikwa Wema alionekana akiwa karibu sana na mwanaume anayefahamika kwa jina la Mkongo (Yule anayempaga jeuri ya fedha) na wakati sherehe ikiendelea, Idris naye alifika bila kujua kuwa alikuwa hatakiwi kuingia ndani.
“Unajua Wema alikuwa na yule Mkongo, sasa wakati Idris anafika getini akashangaa anaambiwa asiingie ndani, Madam ndiyo kasema hivyo na akaambiwa yeye wataonana hotelini.
“Inavyoonesha Wema hakutaka kuwagonganisha kwa hiyo ilikuwa ni lazima acheze kama Pele kuhakikisha Idris haingii ndani na kutibua mambo.
“Idris wa watu ambaye alikuwa akijiandaa kupaki gari akawa hana jinsi, akageuza na kuondoka,” kilidai chanzo hicho.
Ikazidi kudaiwa kuwa, hata baada ya pati Wema hakwenda kule hotelini kuonana na Idris kama alivyosema, badala yake yeye, Mkongo na kampani yao walielekea Maisha Club ambako walikula bata hadi kuchwee.
- Idris anasemaje?
- Wema je?
No comments:
Post a Comment