Thursday, 5 May 2016

TIMU YA AZAM FC YANYANG'ANYWA POINTI 3 DHIDI YA MBEYA CITY



TIMU ya Azam FC, imepokwa pointitatu na mabao matatu kutokana
na kumtumia beki wao, Erasto
Nyoni aliyekuwa na kadi tatu za
njano.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),
Alfred Lucas, amesema katika
mechi namba 156 iliyozikutanisha
Mbeya City dhidi ya Azam kwenye
Uwanja wa Sokoine, Mbeya, Azam
ilimchezesha Nyoni kinyume na
sheria huku wakitambua kufanya
hivyo ni kosa kisheria.
“Azam wamepoteza mchezo ule na
sasa Mbeya City imepewa pointi
tatu na mabao matatu pia
tumelipa onyo benchi la ufundi la
Azam kuwa makini ili jambo hili
lisiwatokee tena,” alisema Lucas.

No comments:

Post a Comment