Mwanamke mmoja
Oliver Erasto mwenye umri wa miaka 22 kabila mchagga mkazi wa Kawe jijini Dar
es Salaam pamoja na mtoto wake wa kiume mwenye umri
wa miaka 3, Emmanuel Erasto, Wameuawa kikatili kwa kuchinjwa na mapanga juzi tarehe 04 May 2016 majira ya saa 12:30 jioni huko eneo la Kaole kata ya Dunda
wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani.
Kwa mujibu wa
kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani alisema mume wa marehemu bwana Erasto Peter
Mbwale mwenye umri wa miaka 26 kabila Mhehe mkazi wa Kawe jijini Dar es Salaam
, akishirikiana na Rafiki yake Rajabu Juma miaka 20, mkulima mkazi wa Makongo
jijini Dar es Salaam, alimdanganya mkewe kwa kumrubuni kuwa wakaangalie ujenzi
wa nyumba yao huko maeneo ya kaole, Bagamoyo akiwa amekodi pikipiki namba MC
235 AWR aina ya FEKON.
Walipofika
kaole, waliingia vichakani mita 100 kutoka barabarani na kuanza kuwaua mkewe
Oliver na mwanae Emmanuel kwa Kutumia mapanga, na kisha kutoroka kwa kukimbia
kutoka eneo la tukio, hata hivyo kelele za marehemu ziliwafanya wakazi waliopo
karibu ya eneo hilo la tukio kusogea karibu kuangalia kulikoni na kelele hizo
ndipo walipokuta miili ya marehemu hao na kutoa taarifa polisi.
Polisi
walipofika eneo la tukio walikuta pikipiki hiyo iliyotumika kwenye tukio hilo,
simu mbili za mkononi zenye line mbili na mapanga mawili yaliyotumika kwenye
tukio hilo la mauaji, ndipo walipoanza msako wa kuwasaka wauaji hao kwa
kuzifuata nyayo zao kutokana na eneo hilo kuwa na matope na hatimaye kwa
kushirikiana na wananchi walifanikiwa kuwatia mbaroni watuhumiwa hao majira ya
saa 3.30 usiku hukohuko kaole wakijaribu kutoroka.
Polisi wanasema
chanzo cha mauaji hayo ni wivu wa kimapenzi baada ya mume bw. Frowin Peter
Mbwale kumtuhumu mkewe kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanaume mwingine
aliyefahamika kwa jina moja la Hamza mkazi wa Kawe jijini Dar es Salaam, na pia
kutuhumu kuwa hata mtoto huyo sio wake bali ni wa Hamza.
Watuhumiwa wote
wametiwa mbaroni jalada la kesi ya mauaji limefunguliwa kwa BAG/IR/1078/2016,
na taratibu za kisheria za kuwafikisha mahakamani zinaendelea.
TAFADHALI PICHA ZINATISHA
No comments:
Post a Comment