Mrembo huyo aliyeuza nyago kwenye Video ya Wimbo wa Kwetu wa msanii wa Diamond, Irene’ Lynn’.
Mrembo ambaye wiki mbili zilizopita aligeuka gumzo baada ya kudaiwa ‘kuchepuka’ na staa wa Afro-Pop, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Irene’ Lynn’ kisha kuleta mtikisiko kwa mpenzi wa msanii huyo, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ amefunguka kuhusu ishu hiyo.Staa wa Afro-Pop, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, akiwa na mpenzi wake Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’.
Akizungumza wikiendi iliyopita baada ya kubanwa aseme ukweli kama anatoka kimapenzi na Diamond, mrembo huyo aliyeuza nyago kwenye Video ya Wimbo wa Kwetu wa msanii wa Diamond aitwaye Raymond alisema kuwa hata yeye ishu hiyo inamshangaza.
Irene’ Lynn’.
Irene alisema siku zote watu hawajiamini wanapomuona msichana mzuri akifanya kazi na mtu fulani na mara nyingine humwekea wivu na kuibua mambo mengine. Irene aliweka wazi kuwa kilichompeleka Wasafi ni kufanya kazi ya Wimbo wa Raymond na hakuna kingine kilichoendelea.“Mkataba wangu na Diamond uliisha baada tu ya kufanya video ya msanii wake,” alisema Irene. Mrembo huyo alitiririka kuwa ishu hiyo inamtesa na kumsumbua kwa sababu watu wengi wanajua kuwa ni kweli ametembea na Diamond, jambo ambalo si kweli.
Skendo ya Irene kutembea na Diamond ilileta mtafaruku mkubwa kwenye familia ya mwanamuziki huyo kiasi cha dada wa mwanamuziki huyo, Esma Platnumz, kuingia kwenye mgogoro mzito na Zari ikielezwa kuwa mrembo huyo ni rafiki yake na alijua kilichokuwa kikiendelea.
No comments:
Post a Comment