Siri
nzito! Ndivyo unavyoweza kusema kufuatia kuvuja kwa picha za mzazi mwenzake na
staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarina Hassan ‘Zari The
Bosslady’ na mtalaka wake, Ivan Ssemwanga wakiogelea kwenye bwawa moja nchini
Afrika Kusini ‘Sauz’.
CHANZO
CHAVUJISHA UBUYU
Kwa mujibu wa chanzo makini kutoka Sauz, wawili hao wamekuwa
wakiwasiliana mara kwa mara, kitu ambacho kimechagiza zaidi uwepo wa siri nzito
ukiachilia mbali kuvuja kwa picha hizo mitandaoni. “Tulikuwa tunawafuatilia
sana hususan kipindi hiki ambacho Diamond hayupo huku Sauz, Zari anaonekana
kuwa na mawasiliano ya karibu na aliyekuwa mume wake, Ivan kitu ambacho kila
mmoja anaamini huenda kuna kitu kinaendelea.”
AZUNGUMZIA PICHA
Chanzo hicho kilizidi kutiririka kuwa, picha tofauti zilizovuja hivi
karibuni za wawili hao wakiogelea katika ‘swimming pool’ maarufu kwa jina la
Soulstice Day Spa, zimezidi kudhihirisha kuwa, wawili hao wana jambo lao kwani
hata kama hawajaweka picha ya pamoja lakini kila mtu kaweka picha yake akiwa
katika bwawa hilohilo. “Kwa kweli lazima maswali yawepo. Je, waliambiana kuweka
picha hizo kwa kupishana muda au kila mmoja aliweka bila kumuuliza mwenzake?”
Inaonesha kabisa walikuwa pamoja au walikutana pale. Kama walikutana pale
walitakiwa mmoja asiweke. “Lakini pia huenda walipeleka watoto japokuwa kwenye
picha hawapo. Hawa wana siri nzito
ambayo Diamond atakuwa haijui,” kilisema chanzo hicho na kuongeza: “Unajua
bora haya matukio wakati yanatokea Diamond angekuwepo huku Sauz wala
tusingetilia shaka lakini haiwezeni waonekane kwenye bwawa moja Sauz halafu
Diamond yuko zake Bongo na naamini atakuwa hajui chochote kinachoendelea.”
MAGARI
NAYO YATAJWA
Kama hiyo haitoshi, chanzo hicho kilikwenda mbele zaidi kwa kudai kuwa,
ukaribu wa Zari na Ivan si wa kutia shaka sana kwa sababu wamezaa. Watoto
watatu si jambo dogo. Lakini kuna habari kwamba, hata magari tofauti ya
kifahari
waliyoyanunua wakiwa kwenye ndoa, wawili hao wameendelea kuyatumia pamoja ila
kila mmoja kwa wakati wake. “Kuna wakati inasemekana Zari amekuwa akitumia
magari ambayo anaonekana nayo Ivan kwa nyakati tofauti hivyo unaweza ukaona
namna walivyo na ukaribu mkubwa,” kilisema chanzo hicho.
MWINGINE AELEZA TOFAUTI
Hata hivyo, chanzo kingine nchini humo kiliwatetea wawili hao kwa kusema
ukaribu wa Zari na Ivan ni wa kawaida kwani hawawezi kuishi mbalimbali wakati
wamezaa watoto watatu pamoja hivyo lazima wawahudumie pamoja.
“Mimi ninavyojua, ukaribu wao ni wa kawaida maana mapenzi yalishaisha
miaka mingi iliyopita na kwa sasa wanawahudumia watoto kwa pamoja, hawataki
watoto wao wapate malezi ya upande mmoja,” kilisema chanzo kingine.
DIAMOND HUYU HAPA
Ili kuweza kujua mbivu na mbichi, paparazi wetu alimvutia waya Diamond ili
kujua kama ana taarifa za mzazi mwenzake huyo kuogelea katika bwawa moja na
aliyekuwa mume wake. Staa huyo alisema amegundua mchezo mchafu dhidi yake na
kwamba kwa sasa hali hiyo haimsumbui. Risasi Jumamosi: Kwanza Diamond utuambie
kama uko Dar au Sauz? Diamond: Nipo Dar, niambie! Risasi Jumamosi: Kuna taarifa
zinazotiliwa shaka kuhusu shemeji yetu, Zari kwamba ameposti picha zikimwonesha
akijiachia kwenye bwawa moja kule Sauz ambapo siku mbili baadaye, Ivan naye
ameposti picha inayoonesha naye alikuwa kwenye bwawa hilohilo, unalizungumziaje
hilo. Diamond: Unajua nimegundua kuna mchezo mchafu unafanywa ili kuniumiza.
Nimeshajua lengo lao hivyo hainipi shida. Huyo mtu (Ivan) anahangaika na mimi
ili nijibu nimpe umaarufu ndiyo maana kwa kipindi kirefu nilikuwa niko kimya.
“Si huyo tu, kuna makundi f’lani hivi kwenye mitandao, wakiona vitu kama hivyo
wananisakama ili mimi niseme au sijui niaibike, ninajua hiyo michezo hivyo
haitanisumbua kamwe. Risasi Jumamosi: Vipi lakini mbona picha zinaonesha eneo
alilokuwa Zari ndilo hilohilo alilokuwa Ivan? Diamond: Huo ni uhuni tu kaka,
hamna ukweli katika hilo.
IVAN ADAIWA KUWA MCHOKOZI
Hata hivyo, baadhi ya watu wamekuwa wakisema kuwa, hali halisi inaonesha
Ivan amekuwa mchokozi kwa mambo kama hayo ili Diamond alie wivu. “Kama Ivan
aliogelea sambamba na Zari hakutakiwa kuziweka picha zile mtandaoni, ule ni uchokozi
tu,” kilisema chanzo kimoja.
CHANZO: RISASI JUMAMOSI
No comments:
Post a Comment