Wednesday, 4 May 2016

WIMBO WA CHURA WAMPONZA NSURA,AFUNGIWA KUFANYA MUZIKI

IMG-20160504-WA0012

Mwanamuziki wa Tanzania Snura Mushi a.k.a Snura au Chura amefungiwa kujihusisha na Sanaa Tanzania.
Wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo leo imetangaza kumfungia Snura kujihusisha na masuala ya sanaa hii ni kutokana na Video ya wimbo wake uitwao chura alioutoa hivi karibu kukiuka misingi ya maadili ya kitanzania.
Pia wimbo wake Chura pamoja na video ya wimbo huo vimefungiwa  kutochezwa kwenye redio, TV na pia kwenye mtandao wa Youtube kwa sababu unakiuka maadili.
Taarifa hiyo imetolewa na wizara hiyo kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwenye ukumbi wake wa mikutano wizarani hapo jijini Dar mapema asubuhi ya leo.
Snura Mushi

No comments:

Post a Comment